GET /api/v0.1/hansard/entries/1515852/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1515852,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1515852/?format=api",
    "text_counter": 470,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Gonzi Rai (",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bunge hili. Kwa hivyo, Mhe. Spika, wakati utaenda kupumzika na kuandika judgement yako, ni mpaka tujue tunaelekea wapi. Mwisho, tunaishi kama familia tukiwa hapa Bungeni. Lakini, naomba niulize wale ndugu wanaojiita wafuasi wa Azimio la Umoja-One Kenya Coalition Party, je, mnavyofanya ni ungwana? Wakati wote tunazungumza tukijua kuwa sisi ni jamii moja. Mahakama ilitoa maamuzi, lakini ilipewa maombi 34 na ikajibu machache tu. Hawakujibu maombi sita. Hatujamaliza siku 14 za kukata rufaa. Leo, tayari hapa tuko katika kizimba. Ni kama hatuwezi kusubiri siku 14 za kukata rufaa ndio haya mambo yaletwe. Kwa hivyo, Mhe. Spika, nenda uketi chini, lakini kumbuka kitengo chetu cha mahakama kina njama fiche ambayo hatujui lengo lake. Kwa sababu tunaheshimu mahakama, tutakata rufaa na matokeo yake yataongoza mwelekeo wa Jumba hili. Tutamaliza mambo ya Jumba hili, lakini sio watu wa mahakama kuja kutupangia tutakavyokwenda. Nafikiri wanafahamu vizuri hii Nyumba ina kinara ambaye atatoa maamuzi yake kuhusu jinsi tunavyopaswa kuendelea na shuhuli zetu kama Bunge."
}