GET /api/v0.1/hansard/entries/1516286/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1516286,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1516286/?format=api",
    "text_counter": 185,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante Bw. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi nichangie Mswada ulioletwa na Sen. Haji wa Kaunti ya Garissa kuhusu mazingira. Mswada huu utasaidia kaunti zote 47. Siku hizi hatuongei mambo ya mlima bali kaunti 47. Ningeomba Serikali ifuatilie huu Mswada kwani utasaidia kila mwananchi kutoka yule wa chini mpaka wa juu. Mambo ya upanzi wa miti yatatusaidia sana. Nakumbuka tukiwa watoto wakati wa uongozi wa Raisi Moi, kulikuwa na momonyoko wa udongo na upanzi wa miti ulifuatiliwa kwa makini sana. Wale wanaosheherekea kuiba miti kwa misitu saa hii ni miti iliyopandwa wakati huo. Ningeomba tufuatilie mipango iliyokuwa zamani ili kaunti zetu zifaidike. Kwanza, ningeomba upanzi wa miti ufuatiliwe na njia inayofaa. Kaunti nyingi hazina maji ya kutumia kupanda miti. Naunga mkono Mswada huu kwa sababu Kaunti ya Embu iko na sehemu kubwa ya ukame kama Kaunti ya Garissa. Naomba Serikali ya Kenya Kwanza iangalie zile kaunti za ukame ndio tuwe kwa mstari wa kwanza kupata maji kupitia zile dams tulizoahidiwa na Serikali kama Kamumu Dam, Thambana Dam na zile zengine pamoja na water pans . Maji yakipelekwa kwa sehemu ya mlima kama Kiambere na Kianjiru na Ndune, watu watatumia hayo maji na itatusaidia kwa upanzi wa miti. Itasaidia pia shule zote za msingi na sekondari kupanda miti. Bw. Spika wa Muda, nakumbuka zamani nikiwa mtoto mdogo, hospitali zilikuwa mbali lakini mtu akiugua alikuwa anaenda kwa misitu ya zamani na kuchukua hiyo miti na kuifanya dawa na anapona. Naomba huu Mswada wa Sen. Haji uzingatie miti kama hiyo. Kuwe na wanasayansi wanaoweza kuchunguza miti kama hiyo kwani itatusaidia kupata hela, dawa na pia kulinda mazingira. Zamani kulikuwa na momonyoko wa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}