GET /api/v0.1/hansard/entries/1516289/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1516289,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1516289/?format=api",
    "text_counter": 188,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "ya kaunti zetu ama serikali yetu. Saa hii, miti mikubwa inatoka Uganda kuja hapa. Ningeomba mambo ya kukata miti iangaliwe. Ningeomba pia mambo ya ushuru yatiliwe maanani. Kwa mfano, katika kaunti ya Embu, kuna shida ya muguka . Upelelezi ungefanywa tujue kama inaweza kusaidia nchi yetu kupitia kutengeneza dawa. Naunga mkono Mswada huu lakini lazima tuangalie vile miti tunayopanda itatuletea faida gani, magonjwa gani na itatusaidia namna gani. Naomba Serkali ya Kenya kwanza itilie maanani upanzi wa miti. Shule zetu zote ziweze kupanda miti ili hata watoto watakaozaliwa wakute misitu kwa shule zetu. Jambo lengine ni kuhusu kukata miti. Inafaa uwe huwezi kukata miti bila barua ya chifu, security ama wale wanaosimamia misitu. Huu Mswada ni mzuri kama utafuatiliwa kwa njia ya haki. Bw. Spika wa Muda, kama Seneta wa Kaunti ya Embu, naunga mkono huu Mswada kwani utatusaidia kwa mambo ya chakula, afya na ushuru wa kaunti na Serikali Kuu. Pia itatusaidia kupata hela kutoka nchi za ng’ambo ikiwa mazingira yetu yatakuwa mazuri. Bw. Spika wa Muda, wiki mbili zilizopita, Rais wetu alizungumzia kuhusu kujisajili kwa Social Health Authority (SHA) ndio waweze kupata matibabu. Cha kushangaza ni kwamba wiki mbili zilizopita baada ya Rais wa Marekani kuchaguliwa, alisema hakuna pesa ya kutusaidia ili tununue madawa. Kuna miti mingi ikifanywa utafiti ule unaofaa, iwapo nchi za ng’ambo zitasita kutupatia hela, nchini Kenya itakuwa ni rahisi mtu kuingia kwa msitu kutafuta dawa. Turudi kwa tamaduni zetu za utumiaji wa miti shamba. Hivyo basi, ninaunga mkono swala la utunzaji wa mazingira na upanzi wa miti. Ni mimi Daktari Seneta Munyi Mundigi."
}