GET /api/v0.1/hansard/entries/1516296/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1516296,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1516296/?format=api",
"text_counter": 195,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ili nichangie Mswada huu uliopendekezwa kutoka Gatuzi la Garissa. Naungana na Maseneta waliotangulia. Ni dhahiri shahiri ya kwamba mabadiliko ya tabia nchi yamedhuru mazingira yetu sisi kama Taifa hususan katika maeneo yasiyo na maji na ni kame zaidi. Vile vile, katika sehemu zinapokea mvua, zimepokea mvua ya viwango wa kupita kiasi hadi kuharibu mimea ambayo inatarajiwa iwe chakula cha kitaifa. Napongeza kipengele kinachopendekeza kupandwa kwa miti mingi zaidi katika maeneo kame. Hii ni wazi kuwa Rais alipoingia mamlakani, alitenga siku moja ya kitaifa na kuiweka huru ili taifa nzima lipande miti. Katika Kauli yake mbiu, alipendekeza wakati tunakata keki siku zetu za kuzaliwa, tusikate keki bali tupande miti ili kuhakikisha vizazi vijavyo vinajivunia kwa yale ambayo tumewatayarishia kuhusiana na mabadiliko tabianchi. Ningependa kuwapongeza washikadau tofauti katika gatuzi yangu ya Mombaa. Akiwemo Mbunge wa Jomvu Mhe. Bady Twalib akishikiriana na Wizara ya Usalama wa Ndani. Mpaka sasa wamepanda miti takriban laki moja katika maeneo ya Ganahola Creek. Bila kumsahau kakangu Amarba Wazir ambaye amejitolea kuhakikisha kwamba gatuzi yetu ya Mombasa imepandwa miti mingi Zaidi. Pia siwezi sahau waziri wangu wa kaunti wa mabadiliko tabianchi Bi. Emily. Natumaini utapata ujumbe huu. Ulikuja kwa ofisi yangu ya Seneta maalum na ukataka ushirikiano. Mombasa ni gatuzi ndogo ambayo haina sehemu nyingi ya kupanda miti lakini kwa kauli yako mwaka wa 2023 tulishirikiana na wakfu wa Mama Haki kuweza kupanda miti 200 katika maeneo ya Kikoani Cemetery. Hii ni kuonyesha jitihada na umoja baina ya viongozi wa Serikali Kuu na serikali ya ugatuzi, kuhakikisha tumefikia ruwaza ya kupanda miti billioni moja katika taifa letu la Kenya. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}