GET /api/v0.1/hansard/entries/1516297/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1516297,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1516297/?format=api",
"text_counter": 196,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika wa Muda, kuna mapendekezo ya kwamba katika gatuzi zetu arubaini na saba kwenye Mswada huu tuweze kuwa na nursery. Nimefurahi sana kuona kwamba sisi kama Bunge la Seneti, tumeoanisha malengo yetu kama wasimamizi wa magatuzi arubaini na saba. Kuona kwamba tunafikia ruwaza ya kiulimwengu. Mabadiliko ya tabianchi hayatudhuru sisi kama taifa la Kenya, bali yanadhuru mataifa ulimwenguni. Tusipojipanga kuweza kutunga sheria kama hizi, na kwa vitendo tutaangamia kama ulimwengu. Baada ya uteuzi wangu, niliweza kuwa na azma ya kupanda miti milioni moja katika gatuzi sita za mkoa wa zamani wa pwani. Nashukuru kwa ushirikiano na taasisi tofauti pamoja na wakurugenzi wa wakfu wangu. Tuliweza kupanda miti maeneo ya Dongo Kundu. Kwa hakika sisi kama viongozi wa kisiasa, tumeambiwa na kuimbiwa wimbo kwamba ni tabia yetu kufanya jambo kupiga picha na kuondoka. Kwa sababu nilikuwa na ari, nilitafuta vijana wa kike ambao waliweza kutelekezwa kwa kupata mimba za mapema. Niliwabunia ajira na nimekuwa nikiwalipa kiwango cha shilingi mia mbili kila Ijumaa waangalie miti tuliyopanda na kuinyunyizia maji. Hivi karibuni nilitembelea Wizara ya Ulinzi na tukakaa chini na Waziri. Tulikubalina kuwa, badala ya kuzunguka kila mahali kutafuta mahali pa kupanda miti ambayo inakuwa changamoto. Kama wakfu wa mama haki, kutambua eneo la ziwa ambalo liko maeneo ya Likoni ili tuweze kupanda miti laki tano; laki moja tutapanda katika gatuzi tofauti. Ninayazungumzia haya kwa mapenzi makubwa kwa sababu sisi ni viongozi. Imesemekana kuwa viongozi ni watu ambao wanastahiki kuangalia maisha ya vizazi vinavyokuja na sio kuangalia kura zinazokuja. Hivyo basi, ningependa kumpongeza kakangu Seneta aliyekuja na Mswada huu. Historia itakukumbuka kwa sababu umetatua tatizo ambalo kwa hivi sasa tunaliona tatizo ndogo lakini ni tatizo kubwa. Ili kufaulu katika hatua kubwa ni lazima tuanze na hatua ndogo. Ninaamini kwamba sheria hii itakapowekwa sahihi na Rais basi kutakuwa na mageuzi makubwa. Na rai kwamba, tutakapokuwa tukitekeleza haya mapendekezo ya sheria, ni pendekezo langu kwamba tuweze kuwaweka vijana wa taifa la Kenya kipao mbele. Wame kumbwa na changamoto ya ajira. Tuweze kuwaweka Watoto wa kike ambao wametelekezwa kwa kupewa uja zito. Wamekosa kuwa na Imani ya kwamba ya kwamba wanaweza kufaulu katika Maisha. Tuwape majukumu ya kusimamia nursery hivi ambazo zitawekwa. Ile miche itakayopandwa iwe ni miche ambayo itasimamiwa na vijana wa kike na wakiume wa taifa la Kenya. Iwe ni njia mojawapo ambayo tumewabunia ajira. Kwa hayo mengi ama machache, hongera kaka na ningependa Bunge hili liweze kubeba kwa uzito mkubwa sheria. Asante Bw. Spika wa Muda."
}