GET /api/v0.1/hansard/entries/1516445/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1516445,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1516445/?format=api",
    "text_counter": 100,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Whip",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Ningependa tu kuwajulisha ndugu zangu kwamba tutaweka kwenye mitandao. Mimi nilikuwa wa kwanza kuwajulisha Maseneta na kuwaambia kuwa kifo cha mzee kimetokea. Hayo yote yaliyotendeka ni mambo ya Mwenyezi Mungu. Tutaendelea kushirikiana na familia ya Spika na ndugu zangu. Mjuavyo, kifo kama hicho sio cha kawaida; ni kifo cha babake Spika wetu na ninajua sisi sote tutajumuika naye. Mimi ninaweza kutangulia nyumbani lakini watakaobaki nyuma mtaendelea kuweka nguvu za Seneti hapo mbele. Jambo la wisho, ingekuwa bora zaidi ikiwa utafafanua hili jambo. Katika ratiba hii ambayo tunasema kuwa sisi tuko katika Broad-based Government na tukijua ya kwamba mahakama ilitoa uamuzi--- Uamuzi huo unahitaji ufafanuzi wa hali ya juu kama alivyosema ndugu yangu Sen. Okong’o Omogeni. Unaweza kufafanua zaidi ili tujue ya kwamba kati ya upande huu na upande ule mwingine, walio wengi ni akina nani? Asante sana."
}