GET /api/v0.1/hansard/entries/1516454/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1516454,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1516454/?format=api",
"text_counter": 109,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, ninaomba viongozi wenzangu waweze kutulia. Wamechangamka kana kwamba wamekula aina fulani ya mmea na mmea huo unaweza kuwa sukuma wiki. Bw. Naibu Spika, nashukuru na ninaombea kila la kheri wale ambao wamechaguliwa na kwamba sisi pia tunataraji kwamba baadhi ya kamati za Bunge zitaweza kushughulikiwa ili ratiba zinazotoka ziweze kuuwiana na vikosi vya uchapakazi, ili tuweze kuwatendea Wakenya haki. Ni lazima kuwahakikishia kuwa popote walipo ya kwamba tutalinda ugatuzi na fedha zao. Uwajibikaji ni lazima ndio Wakenya wafurahie matunda ya ugatuzi. Mimi ninaomba Wakenya mahali popote walipo iwapo kuna tetezi na changamoto wasikose kututafuta sisi Maseneta kwa sababu sisi ndio kio cha jamii. Asante sana, Bw. Naibu Spika."
}