GET /api/v0.1/hansard/entries/1516510/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1516510,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1516510/?format=api",
"text_counter": 165,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Nawapongeza Maseneta wenzangu kutoka gatuzi ya Mombasa, kiongozi wetu Sen. Faki na dadangu Sen. Crystal Asige kwa kuweza kuteuliwa na kutwikwa majukumu ya kukaa kwenye Kamati hii. Bw. Naibu Spika, baada ya kushuka na kuteremka katika mlima kupita katika Bonde la Ufa na kufika Pwani tunashukuru ya kwamba tumerudi tukiwa buheri wa afya. Niliweza kupendekeza katika awamu iliyopita ya Bunge hili tuweze kubuni kamati ya kusimamia ripoti. Ili tuweze kuona utekelezwaji wa yale makubaliano katika kamati zetu. Lakini hatukuweza kukubaliana na kamati iliyochaguliwa safari hii. Nitakuja tena na pendekezo kama hilo ili tuweze kubuni kamati ya kufuatilia zile ripoti tunazopitisha. Ni kinaya kuona kuwa tunaketi kwenye kamati tofauti. Mimi nitakuja na makubaliano ya jinsi ya kutatua lalama na matatizo ya wananchi wa Kenya, lakini hatimaye tunaandika ripoti na zinabaki katika majengo haya ya Bunge la Seneti. Bw. Naibu Spika, ningependa kuchangia katika Hoja inayoendelea. Hapa Seneti tulikuwa na Maseneta wawili walioweza kuchaguliwa na wakaapishwa. Wakati Mhe. Rais aliwachagua kama Waziri, Sen. Okenyuri hakuja tu na kuchukua kiti kwa sababu IEBC iliashiria kuwa awe Seneta. Ningependa kuwakumbusha viongozi wenzangu kuwa hili sio soko la Musangarire ama soko la kule Keroka. Hapa tuko katika Bunge la Seneti ambalo liko na nidhamu zake. Tunasubiri tuweze kupewa mwelekeo na Karani wa Bunge la Seneti. Iwapo kuna hoja yoyote ya upande gani ni ya wachache na wengine ndio walio wengi, tutajulishwa. Haiwezekani watu kujipa mamlaka kama karubandika. Ni kama hapa Seneti tuko na karubandika wa kizazi kipya. Kwa hayo mengi ama machache, ningependa kuwapongeza walioteuliwa katika kamati hii. Walioteuliwa wayape Miswada yetu kipau mbele kuliko yale ya kutoka Bunge la Kitaifa . Hii ni kwa sababu sisi tunapitisha Hoja zetu na zinapofika kule zinawekwa na hazipewi first priority. Asante."
}