GET /api/v0.1/hansard/entries/1516608/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1516608,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1516608/?format=api",
    "text_counter": 263,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, kazi ile iliyobakia katika Bunge letu ni kazi nyingi sana. Ukiangalia zile Petitions, Motions na Statements ambazo zilikuwa zimeratibiwa kabla ya kuenda likizo ilikuwa nyingi sana. Nyingine zilikuwa za Jimbo la Taita Taveta za mambo yanayohusiana na mashamba, Wanyama pori na ukosefu wa maji. Kuna Miswada miwili muhimu sana ambayo yametajwa na Sen. (Prof.) Kamar inayohusiana na elimu na mwelekeo wa Controller of Budget ya kwamba hakuna county inayoruhusiwa kupeana bursary. Pia kulikuwa na Mswada wa Sen. Karungo Thang’wa kuhusu kufanya elimu iwe bure. Hiyo ni miswada muhimu na ya maana sana ambayo yanahitaji Seneti itoe mwelekeo. Kila wakati kunapotokea matatizo katika inchi, Seneti imeitwa kufanya uamuzi wa kupeana mwelekeo kwa nchi yetu. Ninakumbuka wakati wa Corona Virus Disease (COVID-19), kulikuwa na Mswada ambao uliletwa Bungeni na Seneta ambaye sasa hivi ni gavana, Hon. Sakaja kuhusu COVID-19. Mwelekeo ulipatikana na zile sera nyingi za kupigana na COVID-19 zilitokana na Mswada huo. Wakati Gen. Zs waliivamia Kenya, ninakumbuka Mswada uliletwa kwenye Seneti tukaujadili na kupeana mwelekea. Sera nyingi ambazo zilitungwa kutokana na hayo zilitokana na Bunge hili. Saa hii tunavyoongea, Watoto wengi wako nje ya shule. Hawaendi shuleni kwa sababu county governments hazipeani bursaries ama pesa ambayo inapewa watoto ili waende shuleni. Tukizipatia Miswada hiyo miwili kipaa umbele; Mswada wa Sen. (Prof) Kamar pamoja na ule wa Sen. Thang’wa, Kenya itapata mwelekeo kama kweli magavana wanaweza kupeana bursaries ama itangojea mpaka mambo fulani yafaywe na mikataba fulani kati ya serikali ya kitaifa na serikali gatuzi ifanywe ili watoto ambao wanatoka familia maskini waweza kupata zile pesa za kuenda shuleni. Pia kuna Mswada muhimu sana wa marekebisho ya katiba ambayo tayari yametajwa ili kuweka the National Government Constituency Development Fund (NG- CDF), the National Government Additional Allocation Fund (NGAAF) pamoja the The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}