GET /api/v0.1/hansard/entries/1516812/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1516812,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1516812/?format=api",
    "text_counter": 55,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Taita Taveta County, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Haika Mizighi",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana Mhe. Spika, kwa kunipatia fursa hii. Kwanza, ni kweli tuko safarini kuenda kule Addis Ababa; tutaondoka kesho asubuhi. Tunaomba heri zote katika safari iliyo mbele yetu. Sasa hivi, ningependa kutoa ujumbe huu wa rambirambi kwa hayati Leonard Mambo Mbotela. Kwa mujibu wa Kanuni 43(1), nasimama kumuomboleza na kusherehekea maisha yake Mzee Leonard Mambo Mbotela, aliyeaga dunia tarehe 7 Februari 2025. Marehemu Mbotela alikuwa mwanahabari tajika. Uanahabari wake ulikuwa kielelezo cha ubora, uweledi, na uadilifu kwa vizazi vingi vya watangazaji wa habari katika kanda ya Afrika Mashariki. Mhe.Spika, tangu akiwa mdogo, marehemu Mambo Mbotela alionyesha shauku kubwa katika nyanja ya utangazaji. Itakumbukwa kwamba mara nyingi, angebuni na kushikilia chupa kama kipaza sauti na kuiga kwa shauku wasomaji wa habari na wachambuzi wa michezo wa Huduma ya Utangazaji ya Afrika (ABS). Mtindo huu ulikuwa dhihirisho la mapema kwamba marehemu Mambo Mbotela alikuwa na talanta ya utangazaji. Hicho kilikuwa ni kiashiria cha uwezo wa kuwa mtangazaji atakayebobea akikomaa. Mnamo mwaka wa 1964, ndoto za marehemu Mambo Mbotela kujitosa na kubobea katika ulingo wa utangazaji zilianza kutimia alipojiunga na Shirika la utangazaji la Sauti ya Kenya, almaarufu Voice of Kenya (VOK), ambalo sasa linajulikana kama Shirika la Utangazaji la Kenya (KBC). Umaarufu wa marehemu Mambo Mbotela katika fani ya utangazaji ulionekana mara tu alipojiunga na Shirika la VOK. Uweledi wake na sauti yake ya kipekee vilimpa ushawishi katika uwanja wa utangazaji, ikiwemo matangazo ya matukio ya kihistoria katika taifa la Kenya. Marehemu Mambo Mbotela atakumbukwa kwa ugwiji wake wa kipekee katika lugha ya Kiswahili na kwa ujuzi alioutumia kwa ustadi kupitia kipindi chake cha redio cha Kiswahili kilichojulikana kama Je, Huu ni Ungwana? Kupitia kipindi hicho, marehemu Mambo Mbotela aliwamulika viongozi na raia kwa matendo yaliyokiuka maadili ya kijamii, kuwakosoa na kuwahitaji wawajibike. Zaidi ya hayo, ucheshi na ufahamu wake katika kutangaza m’bashara mchezo wa kandanda na sikukuu za kitaifa ulivutia sana wasikilizaji kote nchini, na kuimarisha hadhi yake katika utangazaji kama sauti ya kitaifa. Alikuwa shujaa aliyeaminika katika nchi yetu ya Kenya. Nikimalizia, Mhe. Spika, natoa pole zangu za dhati kwa familia, marafiki na taifa lote nzima kwa ujumla kwa kumpoteza mtangazaji huyu maarufu, Mzee Leonard Mambo Mbotela. Kujitolea kwake katika utumishi wa umma, uweledi na uadilifu katika kazi utabaki kuwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}