GET /api/v0.1/hansard/entries/1516820/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1516820,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1516820/?format=api",
"text_counter": 63,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kaloleni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Paul Katana",
"speaker": null,
"content": " Asante Mhe. Spika. Najiunga na wenzangu kumwomboleza mwandishi shupavu, Leonard Mambo Mbotela. Bwana Mbotela alikuwa kiungo muhimu na kielelezo bora kwa waandishi wa habari, nikiwa mmoja wao. Aliinua vipaji vingi sana vya waandishi, na uboreshaji wa uandishi katika nchi hii. Ingekuwa vyema kama watu wote ambao wametoa mchango mkubwa katika taifa hili kwa usanii na pia waandishi waweze kukumbukwa kabla hawajafa. Leonard Mambo Mbotela alikuwa mtangazaji maarufu na pia mwendeshaji vipindi katika redio ambavyo vimeelimisha watu wengi, kikiwemo kipindi chake cha Je, Huu niUngwana? Ninaiombea roho yake ilale mahali pema peponi. Pia naiombea familia yake iwe na subra wakati huu wa maombolezi. Asante sana, Mhe. Spika."
}