GET /api/v0.1/hansard/entries/1516822/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1516822,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1516822/?format=api",
    "text_counter": 65,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Gilgil, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Martha Wangari",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana Mhe. Spika. Hata mimi nampa hongera Mhe. Haika Mizighi kwa kuleta habari ya kifo cha mwendazake, Leonard Mambo Mbotela. Tukisoma historia, tunajua kuwa Mambo Mbotela hakuwa tu Mkenya. Babu ya babu yake alikuwa ametekwa nyara kule Malawi, ndio wakajipata wamefika kule mwambao. Kwa hivyo, alikua na mizizi sio tu ya Kenya, bali ya Afrika nzima. Hatuwezi kusoma historia ya majaribio ya mapinduzi ya Serikali ya 1982 bila ya kumkumbuka Leonard Mambo Mbotela. Alisomea kule Kitui na kuanza kazi kule Nakuru kama mfanyakazi wa kikundi cha Standard, kabla ya kuenda katika Voice of Kenya (VoK). Yuko na historia nzuri ya zaidi ya miaka hamsini katika kuwapasha habari Wakenya, dunia nzima na Afrika ya Mashariki. Kwa hivyo, tunamuombea dua kwa Mungu amlaze mahali pema na aweze kupumzika kwa amani. Kwa jamaa na marafiki, tunawaombea faraja."
}