GET /api/v0.1/hansard/entries/1516828/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1516828,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1516828/?format=api",
"text_counter": 71,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kitui South, JP",
"speaker_title": "Hon. (Dr) Rachael Nyamai",
"speaker": {
"id": 13374,
"legal_name": "Richard Ken Chonga Kiti",
"slug": "richard-ken-chonga-kiti"
},
"content": "Namkumbuka Mambo Mbotela nilipokuwa mdogo. Wakati huo, redio ilikuwa ni moja, na kwetu tulikuwa wengi sana. Kwa hivyo, tulikuwa tunazunguka hiyo redio tukisikiliza kipindi chake cha Je, Huu ni Ungwana? Alikuwa mcheshi na alifundisha jamii. Pia alifanya kazi nyingi sana katika nchi ya Kenya. Ningependa kukumbuka maneno ambayo Leonard Mambo Mbotela alisema wakati alikuwa amezeeka na amefanya kazi nyingi. Aliuliza kama inawezekana kazi aliyoifanya ihifadhiwe katika museum yetu. Mhe Spika, kama mkubwa wetu katika Bunge, na kupitia Kamati yetu ya habari na mawasiliano, naomba tuzingatie jambo hili na tulipatie uzito ili tuhifadhi kazi ambayo aliifanya ili iwasomeshe watu wengine. Asante sana Mhe. Spika."
}