GET /api/v0.1/hansard/entries/1517163/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1517163,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1517163/?format=api",
    "text_counter": 83,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii. Mimi nasimama kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu Nambari 53(1) ya Kanuni za Seneti, kuomba kauli kutoka kwa Kamati ya Afya kuhusiana na kuzorota kwa huduma za afya katika Kaunti ya Mombasa. Kaunti ya Mombasa inajivunia kuwa jiji la pili nchini na pia kuwa na bandari inayohudumia, kando na nchi yetu, nchi kadhaa za ukanda wa Afrika Mashariki ikiwemo maziwa makuu; Uganda, Rwanda, Burundi, Congo, Sudani Kusini na vile vile Ethiopia. Mombasa ndiyo jiji lenye uwanja wa ndege wa kimataifa katika eneo nzima la kanda ya Pwani na ndiyo makao makuu ya eneo la Pwani. Hivyo basi, ni kaunti ambayo inahudumia watu wengi na serikali ya kaunti inapaswa kujitahidi kutoa huduma kwa kiwango cha hali ya juu. Afya ni huduma muhimu sana na imegatuliwa na ndiyo ilikuwa huduma iliyoboreshwa zaidi na serikali ya awamu ya kwanza katika kaunti hii. Ni masikitiko kwamba baada ya muda wa miaka miwili tu ya serikali iliyoko, huduma zimedorora kuliko ilivyokuwa hapo zamani. Hakuna pesa zozote za serikali ambazo kaunti inatoa kwa vituo vya afya ili kuboresha huduma kwa wananchi."
}