GET /api/v0.1/hansard/entries/1517171/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1517171,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1517171/?format=api",
"text_counter": 91,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "hata walinzi wa milango na maeneo ya hospitali na zahanati nyingi za Kaunti ya Mombasa. (2) Ibaini sababu zilizopelekea Serikali ya Kaunti ya Mombasa kupuuza uboreshaji wa huduma kwa kutoshughulikia miundo mbinu kama vile ukarabati wa majengo ya vituo hivyo, hususan Hospitali ya Tudor ambapo hivi majuzi mgonjwa aliangukiwa na dari wakati anasubiri huduma katika hospitali hiyo. Vile vile, zahanati za Maweni na Ziwa la Ngomo ambazo huvuja na pia hufurika maji wakati wa mvua pamoja na usambazaji wa maji safi ya mifereji. (3) Ieleze hatua ambazo zinachukuliwa na Serikali ya Kaunti kununua na kuboresha vifaa vya kuhudumia wagonjwa kama vile mashine za X-ray, MRI na ambulensi, ikizingatiwa kuwa MRI ya Kaunti nzima inapatikana katika Hosipitali ya Coast General na mara kwa mara mashine hii inakwama kwa sababu ya uwezo mdogo na vile vile kuhudumia watu wengi kwa wakati mmoja. Bw. Naibu Spika, Kaunti ya Mombasa ina ambulance nne pekee zinazofanya kazi kuhudumia kaunti nzima yenye wadi 30 na maeneo Bunge sita."
}