GET /api/v0.1/hansard/entries/1517224/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1517224,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1517224/?format=api",
    "text_counter": 144,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "kwa sababu inahudumia hizo kaunti zote. Tukisikia kwamba hali ya afya katika hospitali hii imedorora basi ni jambo la kuhuzunisha na kutia wasiwasi. Nilikuwa na Mswada muhula uliopita; nafikiri nitaurejesha. Mswada huo ulikuwa unaangalia ni vipi hospitali ya Coast General inawezakuwa hospitali ya rufaa kwa sababu ina umuhimu mkubwa sana. Kaunti ya Mombasa ina watalii wengi. Ni lazima kuwe na huduma za afya za kutosha ambazo na za kiwango cha juu. Jana tuliambiwa na Sen. Miraj kwamba kuna mgonjwa ambaye alitoka hospitali ya Taita-Taveta juu ya ukosefu wa huduma za kujifungua na ikabidi aende hospitali kule Mombasa. Kama hospitali ya rufaa kule ingekuwa nzuri basi angepata matibabu lakini ilibidi aende hosipitali ya Aga Khan ambayo ni private. Pesa ambayo wanadai kutoka kwake sasa ni zaidi ya milioni tisa. Huyu mama alifariki. Bw. Spika wa Muda, ni vyema county governments ziangalie hali ya afya ya hosptali zetu. Sen. Miraj alitoa hoja jana ya kwamba mama huyu hakutibiwa kwa sababu"
}