GET /api/v0.1/hansard/entries/1517234/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1517234,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1517234/?format=api",
"text_counter": 154,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, ningependa kusisitiza kuhusu Taarifa ambayo Sen. Faki ameleta hapa kuhusiana na hali ya afya katika Kaunti ya Mombasa. Coast General Teaching and Referral Hospital ina mapacha katika kaunti tofauti ambao wanafanana kabisa. Tulizungumzia masuala ya matabibu wanaojitolea ambao hali yao ni ya kusononesha sana. Kuna wahudumu wengine katika hospitali zetu ambao kwa wiki kadhaa sasa wamekuwa kwenye migomo, zikiwemo kaunti za Kisii na Bungoma. Kaunti za Nairobi na Mombasa zinafanya mazoezi. Itakuwaje kaunti za humu nchini, ikiwemo Bungoma kuwa na mustakabali ama makubaliano ya kurejea kazini na kwamba kutakuwa na marupurupu ya kununua mavazi, kupandishwa vyeo ama madaraka kwa madaktari kwa wakati unaostahili ilhali wanapouliza kuhusu makubaliano hayo wanatishwa, mishahara yao kusimamishwa na wengine kusimamishwa kazi? Wakati umefika kwa magavana kuwajibika. Viongozi wa"
}