GET /api/v0.1/hansard/entries/1517236/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1517236,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1517236/?format=api",
"text_counter": 156,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "madaktari wako kwenye migomo ilhali magavana hawaoni kama kuna shida katika kaunti zao. Nashukuru Maulana kwa kunipa nafasi kuwa mwanakamati wa Kamati ya Afya katika Seneti. Tukiwa na Sen. Olekina pamoja na wengine tutalivalia njuga suala hili. Tunafaa kutembea katika kaunti hizi, kuwataja kwa majina na kuwaeleza kinagaubaga kadamnasi ya umma wale ambao kwa sasa wako katika nchi za ng’ambo kufanya utafiti na kuzuru miradi ya kule ilhali kwao nyumbani ni aibu tele na haitupi sisi moyo kwamba wao ni magavana. Baadhi ya hospitali zetu hazina dawa. Wamejenga hospitali gushi. Kuna majumba yasiokuwa na matabibu na madaktari. La muhimu ni kuwa wanajenga vyumba---"
}