GET /api/v0.1/hansard/entries/1517238/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1517238,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1517238/?format=api",
"text_counter": 158,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Boy",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13200,
"legal_name": "Issa Juma Boy",
"slug": "issa-juma-boy"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa ambayo imeletwa na Seneta wa Mombasa, Sen. Faki. Kusema kweli, Coast General Teaching and Referral Hospital ni hospitali tunayotegemea sisi kama watu wa pwani. La kusikitisha ni kuwa hivi karibuni, nadhani ilikuwa mwezi jana, kuna kijana mdogo wa umri wa miaka miwili ama mitatu hivi aliyezaliwa katika Kaunti ya Kwale. Mtoto huyo ni mvulana lakini sehemu zake za siri zimeingia ndani sana. Ilibidi apewe rufaa kwenda Makadara. Mimi nilienda nikamwona daktari mkuu, Dkt. Kalwala, ambaye alinisaidia sana."
}