GET /api/v0.1/hansard/entries/1517240/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1517240,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1517240/?format=api",
    "text_counter": 160,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13200,
        "legal_name": "Issa Juma Boy",
        "slug": "issa-juma-boy"
    },
    "content": "mtoto huyo kwa specialis t wa watoto. Ilishindikana kule Mombasa kwa kuwa hakukuwa na daktari ambaye angeweza kumfanyia upasuaji. Kwa hivyo, Taarifa hii ambayo imeletwa hapa na Sen. Faki ni ya muhimu sana. Ikiwa Coast General Teaching and Referral Hospital ni hospitali ya rufaa, inatakikana iwe na madaktari ambao wamebobea na wanaweza kutibu watu. Isiwe kuna mgonjwa ilhali hakuna daktari. Vile vile, utapata kuwa hakuna dawa. Hilo ni jambo la kusikitisha sana. Kuhusiana na kesi ya mtoto huyo, mimi kama Seneta wa Kwale nitajaribu kadri ya uwezo wangu. Nikirudi kule, nitahakikisha kuwa nimemleta mtoto huyo Nairobi ili aweze kupata huduma anayostahili. Kwa hivyo, naunga mkono Taarifa hii iliyoletwa na Sen. Faki."
}