GET /api/v0.1/hansard/entries/1517315/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1517315,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1517315/?format=api",
"text_counter": 235,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante sana Bw. Spika wa Muda kwa kuleta Mswada huu kuhusu mazingira katika Seneti. Nasimama kuunga mkono kwa dhati huu Mswada ambao wewe Seneta jirani Abdul Sen. Abdul Haji umeileta kwa Bunge. Naunga mkono sana hasa kipengele cha sita kinachosema ya kwamba Seneti ikipitisha Mswada huu, kila mwaka kuanzia tarehe 5 hadi 21 Machi tutakuwa na wiki moja ya kupanda miti kama Wakenya. Naanzia mazungumzo yangu pale Seneta mwenzangu wa Kisii, Sen. Onyonka alipokomea. Tukipitisha huu Mswada ya kwamba kila mwaka kuna siku tumeziweka katika mwezi wa tatu za kupanda miti, tutatengeneza utamaduni utakaotuingia katika akili zetu ya kwamba ni lazima tutunze mazingira yetu. Sen. Onyonka amezungumza kuhusu 4K Clubs. Tulipokuwa watoto shuleni, tulikuwa tunaambiwa ni lazima tujenge na tutunze mazingira yetu. Kwa hizi klabu, tulifunzwa matumizi ya miti kadha wa kadha. Kwa mfano, tungeambiwa mti huu ni wa dawa, huu ni wa kivuli, kuzuia maji yasipite na kadhalika. Miaka imepita na watoto hawafunzwi tena mambo haya. Mimi mwenywewe nilipokuwa mdogo, nilisoma Shule ya Msingi Ronald Ngala ambapo baba alikuwa anafanya kazi. Baadaye, nilienda Shule ya Msingi ya Arap Moi- Ngao. Mti nilioupanda miaka ile katika shule yangu ya msingi mpaka leo mti huo upo. Nilipokwenda Shule ya Upili ya Alliance, tulifunzwa ya kwamba huwezi kukanyaga nyasi. Mtu yoyote ambaye amefunzwa hizi tamaduni huwezi kumpata akikanyaga nyasi. Hata mimi leo nikiona leo mahali palipo kijani kibichi, mimi kukanyaga pale ni vigumu sana. Hata kama watu wanapita, mimi hutafuta namna ya kupita nje kwa sababu ya ule utamaduni niliyojifunza nikiwa mdogo. Hivyo basi, tukiweka utamaduni wa kitaifa wa kwamba Wakenya wote ifikapo Mwezi wa Tatu tutakuwa sote tunaenda kupanda miti kwa wiki mzima, serikali zetu za"
}