GET /api/v0.1/hansard/entries/1517317/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1517317,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1517317/?format=api",
"text_counter": 237,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kaunti tukifika Mwezi wa Tatu tarehe 15 sote tunaenda kupanda miti, hili litaleta tabia mpya itakayotusaidia kutunza mazingira yetu. Hii ni tamaduni tunayotaka kuikuza kwa watoto wetu. Leo hii tukiwa tunatembea na watoto wangu niliyowazaa, nikichukua chupa ya plastiki na nijaribu kuitupa, watoto wananiambia, baba hiyo ni tabia mbaya. Kwa nini? Wamefunzwa umuhimu wa kuweka mazingira safi. Sasa huu Mswada tunataka tuunge mkono na kuupitisha. Kwa miaka yote, itakumbukwa ya kwamba Sheria ya Sen. Abdul Haji ndio tunayoifuata. Kila mwaka tukienda kufanya hilo zoezi, tutakuwa tunakukumbuka. Hiki ni kitu kikubwa sana ulichopitisha. Nimefurahi kukuunga mkono. Ukienda katika kila kaunti hususan Kaunti yangu ya Tana River, utakuta kuna nafasi ambazo magavana wemeka miti na kuitengeneza ili wananchi wapate nafasi ya kupumzika pale ama kujivinjari. Lakini kitu ambacho kimenishangaza sana ni kwamba magavana wa kaunti zetu sehemu hizo walizozijenga na kupanda miti zimefungwa. Watu hawaendi huko kujivinjari ama kupumzika tena. Sehemu ya Hola katika Kaunti ya Tana River palipopandwa miti ili kuboresha mazingira yawe mazuri, hakuna watu wanaokubaliwa kuingia. Wanasema ukiingia unaenda kuharibu. Sasa mimi nashangaa, haya mazingira tunayotaka kuyajenga ni kwa nini yasiwe wazi kwa wananchi. Sio Tana River pekee. Hapa Nairobi, kuna hii sehemu inaitwa Uhuru Gardens. Ilikuwa ni mahali pazuri sana ambapo wananchi wengi wanaoishi katika sehemu hiyo walikuwa wanaenda kupumzika. Watu wengi watakuambia walienda na wakapata wachumba wao kule na hata wakafanya sherehe za kuona sehemu hiyo. Sasa Uhuru Gardens imechukuliwa na Serikali hiyo hiyo ilhali pesa za wananchi walewale ndizo zimejenga mahali pale pakubwa pa sherehe. Sasa imekuwa ni Sherehe ya Rais peke yake. Hakuna mwananchi anayekubaliwa kuingia."
}