GET /api/v0.1/hansard/entries/1517529/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1517529,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1517529/?format=api",
"text_counter": 86,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ili nichangie katika Taarifa iliyoletwa na Seneta wa Nairobi ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Orange Democratic Movement (ODM). Ni kweli wahudumu wetu wanaopeana huduma ya Afya, Community Health Promoters (CHP) wanazongwa na changamoto nyingi sana kule mashinani. Ni muhimu serikali za ugatuzi zihakikishe vile vifaa vinavyoletwa na Wizara vimewafikia hawa wahudumu. Wanapambana na changamoto nyingi sana. Ukiniruhusu, najulisha Seneti masaibu ambayo wanapitia wafanyikazi wetu wa gatuzi 47. Yuko mwanadada mmoja aliyeenda kupata huduma ya kujifungua. Alifanyiwa upasuaji katika Gatuzi la Taita-Taveta. Kwa bahati nzuri au mbaya, wahudumu wakalemewa. Msichana yule akapelekwa Hospitali ya Aga Khan Mombasa. Tunapozungumza hivi sasa, mwanadada huyo ameaga dunia akiwa anadaiwa Kshs 9 milioni. Afueni ya kwanza, familia walikimbia katika Idara ya Afya ili wasaidike na Huduma ya Bima ya SHA. Cha kushangaza ni kwamba, gatuzi ya Taita-Taveta imekuwa ikimtoza dada huyu ambaye ni mfanyikazi ada ya SHIF lakini hayajafikishwa kwa taasisi husika. Tunapozungumza, mwili wa mwendazake umelala katika chumba cha kuhifadhia maiti bila hatima yake kujulikana. Ningependa Seneti ambayo hugawa pesa kuzipeleka mashinani, wafanyikazi wa kaunti wanakatwa pesa na ada hizo hazifiki katika taasisi husika. Je, sisi kama Seneti, tutaendelea vipi kupeleka pesa katika gatuzi zetu 47 wakati magavana wananyanyasa wafanyikazi wao? Hili ni jambo ambalo ningependa kakangu Seneta wa Kilifi ambaye pia ni Kiongozi wa Walio Wachache naona unaniangalia. Je, tutawasaidia vipi hawa wafanyikazi? Sisi katika Kamati ya Kudumu ya County Public Investments and Special Funds Committee (CPISF) tulizungumzia kuhusu ada inayotozwa ya malipo ya uzeeni. Lakini ni jambo la kusikitisha kuona ya kwamba mfanyikazi wa Serikali ya Kenya wa gatuzi anatozwa ada na hayaendi katika taasisi husika. Familia inadaiwa milioni tisa wakijua watapata afueni katika Taifa Care ilihali ada iliyotozwa haijafika kule. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}