GET /api/v0.1/hansard/entries/1517542/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1517542,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1517542/?format=api",
"text_counter": 99,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda kwa nafasi hii ya kuchangia kwenye Kauli za Maseneta. Kauli ambayo Sen. Sifuna ameibua, nimekuwa nikizungumzia mara kwa mara. Kile ambacho nimeona matabibu hawa wa mashinani ni kwamba wako na rununu lakini kwenye mikoba ile hakuna dawa wala hamna pesa. Begi zile hazina ala za matumizi kama vifaa vya kupima damu na mambo kadhaa. Tulikuwa Kaunti ya Naivasha tukijadili kwamba iwapo Serikali itaweza kuongeza mgao wa fedha. Tunafaa tukubaliane kwamba fedha hizi zitatoka kwenye serikali kuu na italipa kwa awamu moja au fedha hizi zitaongezwa na serikali za kaunti zitakazolipa wafanyikazi hawa kwa awamu moja. Kile kinachodhihirika wazi ni mchezo wa paka na panya na wale ambao wanaumia ni wafanyikazi waliojitolea lakini wanaongozwa na viongozi dhalimu wasiokuwa na moyo au utu. Wahudumu hawa wanapodai mishahara wanaambiwa hawakuajiriwa na wala hawana mkataba kati yao. Wanaambiwa kuwa wanafanyiwa hisani kwa sababu wao ni watu wa kaunti zao. Kando na kudhibiti mfumo wa kulipa mishahara lazima kuwe na mikataba mahususi ambayo itatia serikali za kaunti au Serikali Kuu kuajibika ili watumishi hawa wa kaunti zetu wahudumie watu wetu kwa njia inayostahili. Hoja nyingine ningependa kufananua ni ambayo ililetwa hapa na Sen. Munyi Mundigi. Alidai kwamba Waziri alitoa ilani kwamba paa za shule za masomo au taasisi za serikali ambazo haziendi au haziafiki mfumo wa kisasa wa paa ziondolewe. Swali ni je, Waziri anapotoa ilani paa zile zitolewe katika taasisi za serikali ametia mpango upi tayari kwa serikali kuziweka kwenye bajeti pesa za kuweka paa mpya? Shule ni taasisi za serikali na hakuna pesa za ziada za shule hizi kubadilisha paa. Iwapo kujenga madarasa, maabara, na vyumba vya kulala vya wanafunzi ni shida itawezekana wabadilishe paa na wakose kuajiri waalimu na ala za matumizi na kadhalika? Naomba serikali kuwa Mawaziri wanapotoa ilani lazima wahusishe jamii katika kuamua miradi ya maendeleo. Haiwezekani kila mara wale kutoa miradi pasipo majadiliano na washikadau. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}