GET /api/v0.1/hansard/entries/1517543/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1517543,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1517543/?format=api",
    "text_counter": 100,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Mwisho kabisa nimeona hoja kuhusiana na Shirika la Reli humu nchini. Hio ni mali ya umma. Watu wamebomolewa vyumba na maeneo ya kazi katika kaunti hizi. Tunachotaka kujua ni kuwa wana mipango ipi ya kuhakikisha kwamba shamba zinazomilikiwa na reli ya nchi ya Kenya yanafanya mujibu wa Katiba? Kwa sababu tuna ugatuzi maeneo gatuzi ya humu nchini yanashirikiana vipi na Shirika la Reli kuwapa wanafanyikazi waliotayari kufanya biashara kwenye shamba ambayo hayatumiki kwa muda mrefu zaidi ya miaka 20? Watu wa mkoa wa magharibi na kaunti ya Bungoma wamesikia nikitaja mambo ya madaktari mashinani. Ninamuomba Gavana wa kaunti hii kwamba tunapozungumza vile ajiandae kwa sababu tunakuja kuwatetea wafanyikazi wetu ili tuhakikishe kuwa wamelipwa mishahara kwa wakati unaostahili; mikataba inaidhinishwa na vile vile kuwe na mazingira mazuri ya kazi katika kaunti ya Bungoma. Nawatakia Wakenya wakati mufti na iwapo wana tetesi, tuko tayari kuwapigania. Asante."
}