GET /api/v0.1/hansard/entries/1517552/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1517552,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1517552/?format=api",
    "text_counter": 109,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Ni sawa ata kama Gavana hatajenga barabara. Afadhali akose kutoa mbegu au pembejeo za kilimo lakini ahakikisha kuwa afya imefikia kila mtu, kwa sababu aliyekufa hatumii barabara zilizoundwa wala kulima. Wanafaa kuwachana na mambo yote ile wanayofanya na wahakikishe kuwa wakaazi wote wako hai. Baada ya kuleta taarifa ambayo tulituma kwenye Kamati ya Afya ambayo inaongozwa na Sen. Mandago, kumekuwa na mambo mengi ambayo yanafanywa kuonyesha kwamba sisi hatujui tunachofanya. Pale kwenye mlango pamewekwa mama na mzee ambao wanakupiga pambaja na kukushika mashavu ili picha zile zirushwe katika vyombo vya habari ionekana kana kwamba magavana wanafanya kazi. Kweli sisi huchaguliwa lakini waswahili husema kibebacho huvuja nafuu kwa mchukuzi. Lakini kama kuna mahali watu wanafaa kuja kuona kifo kwa macho ni idara ya afya kule Kaunti ya Kirinyaga. Ni vizuri madaktari ambao wanahusika kutupea afya na kuhakikisha tuko hai walipwe pesa zao wakati unaofaa ili watuhudumie pia. Wale ni wazazi, wanalipa kodi na pia karo za shule. Asante."
}