GET /api/v0.1/hansard/entries/1517565/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1517565,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1517565/?format=api",
    "text_counter": 122,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante, Bw. Spika wa Muda. Kwanza nampa kongole Seneta wa Nairobi, ndugu yangu Edwin Sifuna, kwa kuleta Taarifa hii ambayo ni muhimu sana kwa watu walio mashinani kote nchini. Jambo la kwanza, ninaiunga hoja hii mkono kwa dhati kwa sababu, wale wanaofanya kazi kule vijijini ni watu muhimu sana na inatakikana waangaliwe na kaunti zao. Ni jambo la aibu kuona hapa Nairobi, ambapo ni jiji kubwa hapa nchini, lina watu wanaojitolea kufanya kazi katika jamii lakini hawangaliwe sawa sawa. Lakini tunasikia kwamba hawaangaliwi, leo watu wanaenda na miguu kavu, hata hawana slippers ama zile viatu ndugu zetu wa Kikamba huwa wanavaa za mpira. Kwa kijaluo, zinaitwa akala . Wanatembea na viatu kama hivyo sababu hawana gumboots kama alivyosema katika Taarifa yake, Katibu Mkuu wa chama chetu cha Orange Democratic Movement (ODM). Hali tetesi kama hizi, hawa watu wanawezapata ugonjwa wakati wowote ama wanapata magonjwa na hawana njia za kwenda kuona daktari sababu hii bima ya Social Health Authority (SHA) haifanyi kazi ama haitambuliwi. Bw. Spika wa Muda, tukiangalia upande wetu wa huko nyumbani Kilifi, kuna jiji kubwa kama la Mtwapa, Malindi, Mariakani, Kaloleni na miji mingine kama Kilifi. Kuna watu pia wamejitolea na ingekuwa muhimu zaidi zile serikali zetu za gatuzi ziangalie hao wanafanya kazi wa kujitolea au kwa jamii ili waweze kuona watapata faida gani, wakijua kabisa wanaangaliwa vilivyo kiafya wakati wowote wakiwa wagonjwa. Tunasema wapewe vifaa vya kufanyia kazi. Siyo wao wanunue wenyewe halafu wanajitolea. Miaka mingi iliyopita, tunajua kuna kina mama walikuwa wanazalisha watu. Hawakuwa madaktari kama Daktari Khalwale. Ndugu yetu Dkt. Khalwale anaweza kutuelezea ya kwamba, tume kuwa na wakunga au wazalishaji wa akina mama. Sio lazima watu waende hospitali. Walikuwa experts. Kulikuwa hakuna haja ya kukatwa"
}