GET /api/v0.1/hansard/entries/1517755/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1517755,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1517755/?format=api",
    "text_counter": 312,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante Bw. Spika wa Muda. Ilikuwa ni mtihani mkubwa sana kufikia hapa ambapo tumefikia kwa sababu kuchagua maseneta na kuwaweka katika kamati hizi zilizoko ndani ya Seneti sio kazi rahisi. Kwa upande wa maseneta walio wachache tumejaribu iwezekanavyo kuona ya kwamba kila tuliyemchagua ni seneta mkakamavu katika kitengo ambacho tumempatia. Mimi ninaunga mkono na kusema kwamba Maseneta hawa wote ambao wamewekwa katika Taarifa hii ya leo wana ujuzi, taaluma, akili na uwezo wa kutekeleza wajibu wa majukumu ambayo tumewapatia. Vile tumewachagua hawa Maseneta ambao watakuwa katika kamati hizi sio kazi rahisi. Mara nyingi tunaona kamati nyingi kwa mfano ule wakati ambao umepita hazikuweza kuendelea na mikutano kwa sababu maseneta wengine walikuwa wakikosekana. Sio kazi rahisi pia kujua maseneta wako na majukumu mengi katika zile nyadhifa wanazotoka katika kaunti zao. Kazi hizo zote wanazozifanya muhimu kwa taifa la Kenya. Hata hivyo, tumekuwa na upungufu wakati mwingine wa kuwa na maseneta wanaokamilika ili kuendesha shughuli za mikutano. Safari hii na muhula huu tuliyonao, hakika hawa tuliyowachagua kutakuwa na mageuzi fulani na watafanya ambavyo inavyotakikana kuona kwamba kamati hizi zinatenda wajibu wao. La mwisho, ninawatakia kila la heri nikiunga mkono orodha hii ya hawa wote ambao tumewaweka hapa. Ninawatakia kila la heri katika haya majukumu. Sio majukumu rahisi lakini wananchi wa Kenya popote walipo wanaangalia kuona ya kwamba, je, Seneti safari hii itatekeleza wajibu wake? Mimi ninaimani na nyinyi nyote Maseneta mliyoko hapa. Kwa upande wa walio wengi na upande wa walio wachache sote tukishirikiana tutaleta sifa yetu ambayo tunajulikana nayo ya kwamba tunaweza kukata kesi na kufanya kazi yake kisawasawa katika kamati zote zilizoko ndani ya Seneti na kuona kuwa haki imetendeka kwa wakenya wote. Asante. Ninaunga mkono."
}