GET /api/v0.1/hansard/entries/1517782/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1517782,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1517782/?format=api",
"text_counter": 339,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante Mstahiki Spika wa Muda. Naanza kwa kuunga mkono wale wote waliochaguliwa hapa katika hizi Kamati zote tatu. Kamati hizi ni nguzo ya Seneti kwasababu ni Kamati ambazo ziko na majukumu ya hali ya juu hususan mambo ya utekelezaji wa pesa na matumizi na pia kuchunguza kama hizo pesa tunazopeleka mashinani zinatumika vyema. Kwa hivyo, tukiwa tunajidai na hizi Kamati, ni kwamba tuko na imani ya kwamba zitatekeleza wajibu wake. Hao waliochaguliwa hapa wote katika hizi Kamati ni wakakamavu. Niko na imani ya kwamba watatimiza vile inavyotakikana kufanywa hasa matumizi ya pesa katika kaunti. Asante. Ninaunga mkono."
}