GET /api/v0.1/hansard/entries/1517810/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1517810,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1517810/?format=api",
"text_counter": 367,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada wa elimu ya uraia ulioletwa katika Bunge na Seneta Okenyuri. Ninampongeza Sen. Okenyuri kwa Mswada huu kwa sababu ni Mswada ambao una mambo mengi mazuri ambayo yatasaidia nchi yetu kuelimisha raia kuhusiana na haki zao, mambo ya kiserikali na majukumu ya viongozi wanaochagua kila baada ya miaka mitano. Katiba mpya ilipokuja mwaka 2010, ilikua ni matarajio ya wengi kua serikali itaanzisha elimu ya uraia, hususan kuelimisha wananchi juu ya haki zao kikatiba na pia yale mambo mengi mapya yaliyokua katika katiba hii yetu. Lakini, ni masikitiko kwamba, haikufanya hivyo. Hii imefanywa kusudi ili kuendelea kuwapoteza raia kuhusiana na haki zao ambazo wako nazo. Bw. Spika wa Muda, kwa mfano, mambo mengi ya elimu ya uraia, yalikua yanadhaminiwa na mashirika ya kibinafsi na yasiyokua ya serikali, yaani the civil society. Ijapokua Katiba ilipopitishwa ilikua ni matarajio ya wengi kuwa, wananchi wataelemishwa juu ya katiba hii na yale mambo na zile sheria mpya zimekuja hio haikutendeka. Kwa mfano, tuna ugatuzi, lakini hatujajua haki zetu kikamilifu kama raia juu ya maswala ya ugatuzi. Kwa mfano, kuna serikali ya kaunti na kuna bunge la kaunti. Lakini, mara nyingi utapata wale wa bunge la kaunti, kama hapa bunge la kitaifa, wanajiona ni pamoja na serikali ya kaunti ile. Wakati majukumu ya serikali na majukumu ya bunge, yamewekwa mbali na bayana kabisa. Kwa mfano, majukumu ya bunge ni kutunga sheria, uangalizi yaani oversight na uwakilishi wa watu. Lakini, utapata katika kaunti nyingi, wabunge wa bunge la kaunti wako mstari wa mbele kuunga mkono yale mambo yanafanywa na zile serikali za kaunti ambayo ni kinyume na sheria. Utapata mbunge wa bunge la kaunti ameongoza watu kwenda kutoa maoni katika vile vikao vya elimu ama vikao vya uhusishaji raia au public participation, kuunga mkono swala ambalo yeye mwenyewe akilini mwake hajaliewa. Utapata vikao vingi vya uhusishaji umma vinafanywa bila kuandaa kikamilifu wananchi wa sehemu zile. Kwa mfano, iwapo mkutano utafanyika leo kule Mombasa, jana jioni ndiyo walituma ajenda ambayo itajadiliwa katika mkutano ule. Hiyo inafanya raia kukosa mchango wowote wa kutoa wakati mambo hayo yanayojadiliwa na mara nyingi wakiulizwa huwa wanasema tumepitisha ama tumekubali na mambo yanakwisha. Mswada huu utatoa mfumo utakao wawezesha wananchi kusoma katiba yao mara kwa mara. Vile vile utawapa wananchi nafasi kujua haki zao katika serikali za kaunti na pia Serikali za Kitaifa. Pia, Mswada huu una lengo la kuwezesha kubadilisha mfumo wetu wa kisiasa. Wananchi wakuwa wanajua ni sababu gani tunachagua viongozi na ni yapi majukumu ya viongozi wale. Mswada huu pia utasaidia raia kujua haki zao kikamilifu. Katiba yetu ina haki karibu hamsini na moja. Ukiangalia kutoka kifungu cha kumi na tisa hadi kifungu cha The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}