GET /api/v0.1/hansard/entries/1517811/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1517811,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1517811/?format=api",
    "text_counter": 368,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "hamsini na moja. Hizo zote ni haki ambazo wananchi wanatakikana wazijue na kuzifuatilia. Kwa sasa wengi watakuambia kuwa haki waliyonayo ni haki ya kuishi, Haki ya Elimu na Haki ya Kujieleza (Freedom of Expression). Zile zingine zote arobaini na nane wananchi hawazijui. Kwa mfano, sasa hivi kuna vyakula vingi ambavyo vinauziwa wananchi wetu lakini hawajui vipi wataweza kujitetea haki zao iwapo vitu walivyovinunua vina madhara kwa binadamu. Vile vile, Mswada huu utasaidia wananchi kutaka huduma nzuri zaidi kutoka kwa viongozi. Hii ni kwa sababu, ukishajua haki yako, utaweza kujua ni njia gani ambayo utatumia kufuatilia haki zile ili ziweze kutekelezwa. Sheria hii pia itawapa majukumi serikali za kaunti na pia serikali ya kitaifa kufanya mikakati ya kuelimisha raia. Kwa sasa, hakuna mikakati yoyote ambayo serikali imeweka kuelimisha raia kuhusu mambo ambayo yanatendeka serikalini na vile vile katika nchi kwa jumla. Jukumu hili pia litatokea kwa kila kiongozi ambaye atachaguliwa awe ni wa kitaifa au wa serikali gatuzi. Atakuwa na jukumu la kufanya kuhusu elimu ya uraia kuhusiana na majukumu yao na mambo mengine inayohusu wafanyikazi wa serikali. Hayo yamo katika Kifungu cha tano ambacho ni muhimu sana. Hivi sasa wengi, na pia hata sisi Wabunge na Maseneta, hatujui majukumu yao. Utapata gavana anakwenda katika hafla akiandamana na wabunge wote wa Bunge la kaunti. Na unapoangalia mambo ambayo wamekwenda kufanya pale, hayahusiani kabisa na majukumu yao. Vile vile wabunge wa kaunti wanashindwa kuuliza gavana maswali kuhusiana ya kazi ambayo wanatakikana wafanyiwe na serikali gatuzi. Mswada huu utatoa fursa nzuri ya kuelimisha viongozi wanapochaguliwa ili wasifuje mali ya uma kama inavyoendelea kwa sasa katika inchi yetu. Vile vile, hii itawapa nafasi nzuri ya kuwapima viongozi iwapo wanafanya kazi yao sawasawa ama hawafanyi kazi vilivyo. Vikundi vile ambavyo vitafanya majukumu yao vimezungumziwa katika Kifungu cha saba na kile cha nane. Kifungu cha tisa kinasema kwamba- “Ni jukumu la serikali ya kaunti kutenga kiwango fulani cha bajeti yake kila mwaka ili kufanikisha elimu ya uraia” Mhe. Spika wa Muda, jukumu hili lazima liwekwe kwa bajeti ya Serikali Kuu. Nimeambwa jana kwamba bajeti ya mwaka ujao itakuwa takriban shilingi trillioni nne nukta mbili. Lazima kuwe na kiwango kitakachotengwa kutokana na bajeti hiyo ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata elimu ya uraia kuhusu majukumu yao na haki zao katika serikali yetu ya Kenya. Pia tumeona kwamba serikali kuu itakuwa na nafasi ya kutoa conditional grants kwa serikali za kaunti ili ziweze kukuza vipaji na kuwa na uwezo wa kufanya elimu ya uraia. Pia kuna kuandikishwa kwa wale watakaotoa elimu ili isiwe inatolewa bila mpango wowote. Kwa hakika Mswada huu utasaidia pakubwa kujenga ugatuzi na elimu katika nchi yetu. Mhe. Naibu Spika, nimeona pia kutakuwa na nafasi ya Waziri kutengeneza searia andamizi ili kuhakikisha haya yaliyozungumzwa katika Mswada huu yanatekelezwa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}