GET /api/v0.1/hansard/entries/1517875/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1517875,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1517875/?format=api",
"text_counter": 52,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Sifuna",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13599,
"legal_name": "Sifuna Edwin Watenya",
"slug": "sifuna-edwin-watenya"
},
"content": "Asante sana, Mstahiki Naibu Spika. Wakati kama huu sio wakati wa mzaha kwa sababu ni lazima tuwape wale ndugu zetu ambao wametuaga heshima yao. Ninataka niichukue fursa hii, kwa niaba yangu, haswa mimi kama kiongozi anayetoka kwa jamii ya Mulembe, na kwa niaba ya wakaazi wote wa Nairobi, pamoja na familia yangu, nitoe rambi rambi zangu kwa mwenda zake, Mhe. Malulu Injendi, Mbunge wa Malava. Ningependa habari hizo ziwafikie ndugu zangu wote katika Bunge la Kitaifa ambao walikuwa wanafanya kazi kwa karibu na Mhe. Malulu Injendi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}