GET /api/v0.1/hansard/entries/1517876/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1517876,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1517876/?format=api",
    "text_counter": 53,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Sifuna",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13599,
        "legal_name": "Sifuna Edwin Watenya",
        "slug": "sifuna-edwin-watenya"
    },
    "content": "Kwa muda mchache ambao mimi nilipata kujumuika naye, ninatoa ushuhuda ya kwamba alikuwa ni mtu mpole sana na hakuwa na shida na watu. Jambo hili ambalo limefanyika ni la kuvunja moyo sana lakini tunaomba kwamba yeye atapata kupumzika mahali pema na kwamba familia yake itapata kufarijika. Mimi nikiwa Katibu Mkuu wa Chama cha ODM, ninajua ya kwamba wakati mwingine tunapojiingiza katika siasa pale chini, huwa zinakuwa zimechacha kweli. Uchaguzi wa mwaka 2022 ulikuwa na dhoruba nzito sana ya wana-Azimio katika Kaunti ya Kakamega. Kati ya maeneo Bunge kumi na mbili katika Kakamega, Azimio waliweza kuzoa jumla ya viti kumi. Ni viti viwili tu; ile ya Shinyalu na hii ya Malava ya Mhe. Malulu Injendi ambayo wana-Kenya Kwanza waliweza kutubwaga. Inaashiria ya kwamba huyu jamaa alikuwa sio mchache ya kwamba, kwa muda huo wote ambao amewatumikia watu wake wa Kakamega, kweli walikuwa wanamuenzi. Kwa hivyo, kwa niaba yangu na kwa niaba ya Chama cha Orange Democratic Movement (ODM), makao makuu ya chama, kinara wangu, Mhe. Raila Amolo Odinga, na watu wa Nairobi, poleni sana kwa kumpoteza mpendwa wenu. Mungu aweze kumrehemu. Asante sana."
}