GET /api/v0.1/hansard/entries/1517886/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1517886,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1517886/?format=api",
"text_counter": 63,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Omogeni",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13219,
"legal_name": "Erick Okong'o Mogeni",
"slug": "erick-okongo-mogeni"
},
"content": "Kwa muda ambao nilimjua Mhe. Malulu Injendi, alikuwa mtu aliyependa kutumikia wakaazi wa eneo Bunge la Malava kwa dhati. Kwa hivyo, natuma pole zangu kwa familia yake, wakazi wa Malava, wale ambao alikuwa anashirikiana nao Bungeni, na taifa lote kwa jumla. Tunapopitia wakati huu wa majonzi, kile tunaweza kufanya ni kuomba na kuweka familia yake mikononi mwa Mwenyezi Mungu awafariji wakati huu mgumu wanaopitia. Tunawahakikishia kwamba sisi kama Bunge la Taifa, Seneti na Parliamentary ServiceCommission, tutashirikiana na familia kuhakikisha kwamba tunapunguza mzigo kwa familia. Tunatuma rambirambi zetu kwa watu wa Malava na Kaunti ya Kakamega. Tunawaombea Mwenyezi Mungu awe nao wakati huu wa majonzi."
}