GET /api/v0.1/hansard/entries/1518012/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1518012,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1518012/?format=api",
"text_counter": 189,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa nafasi hii ambayo umenipa kutoa rambirambi na pole zangu kwa familia ya Cheptumo. Ningependa kusema kwamba Mhe. Cheptumo nenda salama. Mhe. Cheptumo, mauti yamekuvika njuga. Nenda salama, shujaa. Unakokwenda hatujui, lakini Mungu anajua. Mhe. Cheptumo, umepigana vita hapa katika Seneti kupambana dhidi ya magaidi, waporaji wa mifugo ya watu wako kule nyumbani. Umetunga sheria na Katiba mpya ambayo tunatumia sasa. Mhe. Cheptumo, umekuwa baba, uti wa mgongo wa familia. Shujaa Cheptumo, nenda salama, tutakutana baadaye. Mhe. Cheptumo, palipokuwa na bughudha na joto la kisiasa hapa Seneti, ulituliza boli. Ulitupa mawaidha, ukatwambia kwamba hasira za mkizi ni furaha ya mvuvi. Sasa umetuwacha wapweke. Umetuwacha na simanzi. Umetuwacha tukibubujikwa na machozi wakati huu mgumu wa kisiasa. Nenda salama. Wasalimu waliotangulia hapa Seneti. Waambie tutafuata nyayo zao siku moja lakini kwa sasa tutafuata yale uliyotangulia. Safiri salama Cheptumo tutakutana baadaye. Katika usanjari huo, ningependa pia kutoa rambirambi zangu kwa familia ya Mhe Malulu Injendi ambayo imepoteza watu watatu; ndugu mkubwa wa Malulu Injendi, Malulu mwenyewe na dadake, muda mchache uliopita amekata roho katika hospitali kule Kakamega. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}