GET /api/v0.1/hansard/entries/1518013/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1518013,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1518013/?format=api",
"text_counter": 190,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Mhe. Malulu ulisomea chuo kikuu nilichosomea. Uliweza kuwa mwenye kiti almashauri na bodi za shule nikiwa mwalimu. Ulipigania watu wako, ujenzi wa miundo mbinu shule na barabara. Ulikuwa mkatoliki wa imani. Tulitunga sheria za ufugaji na upanzi wa miwa na usagaji wa sukari tukitaraji kuwa wakulima wako wa Malava watanufaika. Tulikuwa kwako na Mhe. Rais. Tukapeana shule ya nua ya Chanderema. Wewe ulikuwa unajua ya kwamba watoto wetu wakinufaika katika masomo, siku zao za usoni zitakuwa salama. Mhe. Malulu, tembea salama. Luwere luwere mwana wa mama, tutakutana Mungu akipenda. Asante sana na Mungu awalinde."
}