GET /api/v0.1/hansard/entries/1518017/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1518017,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1518017/?format=api",
    "text_counter": 194,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dkt.) Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili niweze kutoa rambirambi zangu kwa familia ya Seneta mwenzetu aliyeaga dunia. Mimi ni Seneta wa Embu Kaunti. Mimi pamoja na watu wa Embu Kaunti tunasema pole sana kwa watu wa Baringo kwa kuwachwa na yule mliyemchagua. Kulingana na historia tuliyopata leo, Seneta Cheptumo amechaguliwa mara nne. Pole kwa watu wa Baringo kwa sababu kuchagua mtu mihula minne sio rahisi. Inamaanisha alikuwa anafanya kazi na wizara zote, akina mama, wazee, watoto na makanisa yote. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}