GET /api/v0.1/hansard/entries/1518018/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1518018,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1518018/?format=api",
    "text_counter": 195,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dkt.) Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Ningeomba watu wa Baringo wavumilie yale yametendeka kwa sababu tunajua katika ulimwengu huu, hakuna mtu ataishi milele. Sisi sote tutaenda. Ningeomba watu wa Baringo waiombee familia ya Mhe. Cheptumo. Ya pili ni kuomba watu wa Baringo, wakati uchaguzi utafika, waweze kuchagua shujaa kama Seneta Cheptumo. Nakumbuka mwaka wa 2002 wakati tulichaguliwa, alikuwa anang’ang’ana na kigogo wa siasa ambaye ni mwana wa hayati Rais Moi na aliye na pesa nyingi. Watu wa Baringo hawakuangalia zile pesa au familia, bali waliangalia ushujaa wa mtu ambaye angeweza kufanya kazi. Mimi na watu wa Gatuzi la Embu tuko na huzuni sana. Nakumbuka wakati Seneta Cheptumo alipokuwa mgonjwa, Kamati ya Kudumu ya Usalama wa Kitaifa, Ulinzi na Uhusiano wa Kitaifa mara kadha wa kadha ililazimika kuahairisha kuzuru Kaunti za Embu, Tharaka Nithi na Meru kwa sababu ya suala la miraa na muguka. Ni ombi langu kwamba atakayechaguliwa kuchukua nafasi yake katika Kamati hii aweze kufanya mithili ya mwendazake Seneta Cheptumo. Sisi tulikuwa tunamngoja sana. Wakati ule Kamati aliyokuwa mwenyeketi ilipanga kuzuru kaunti zetu, akawa mgonjwa na vikao vya kamati vikahirishwa. Tuko na huzuni lakini kifo hakisimamishwi. Ingekuwa deni ya hospitali, sisi tungechanga. Hivyo basi, mimi Seneta wa Embu na wananchi wa Embu tunatoa rambirambi zetu kwa wananchi wa Baringo. Natoa pole zangu kwa familia na wananchi wa Malava kwa kumpoteza Mbunge wao, mheshimjiwa Ijendi. Kati ya Wabunge ninaowajua kwa Bunge la Kitaifa, mmoja wao ni Mheshimiwa Ijendi. Ni Mtu aliyekuwa na ushujaa wa mambo ya kanisa. Tulijuana na yeye tukiwa kwa masuala ya kanisa. Kwa wananchi wa Malava, poleni sana. Kwa kweli kifo hakizoeleki. Basi Mwenyezi Mungu awafariji. Nawaomba wakaazi wa Malava na Baringo wakati uchaguzi utakapokuja, wachague Mbunge na Seneta mzuri. Poleni sana na Mungu awalaze mahali pazuri hadi siku ya kiama. Wakati Yesu Kristo atakapokuja nasi sote tutafufuka na wao. Asante sana. Ni mimi Daktari, Sen. Munyi Mundigi, Seneta wa Kaunti ya Embu"
}