GET /api/v0.1/hansard/entries/1518030/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1518030,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1518030/?format=api",
"text_counter": 207,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Kwanza kabisa, kwa uchungu na huzuni nataka kuleta risala zangu za rambirambi kwa familia ya mwenda zake, Seneta William Cheptumo. Bw. Spika wa Muda, nikubalie kabla sijaleta risala zangu za rambirambi, nataka kuchukua fursa hii kutoa shukrani kwa Seneti pamoja na wafanyakazi wote wa Seneti na Bunge la Kitaifa. Hii ni kwa sababu juzi nilimpoteza babaangu, Seneti na wafanyakazi wa Bunge walisimama nami. Sitaki kuchukulia jambo hilo kwa mzaha. Nataka kuwashukuru kutoka pangu rohoni na niwaambie asante na asante sana. Uchungu nilionao wa kumpoteza mzazi ninauelewa vile vile uchungu wa watoto na Mjane wa Seneta wetu Cheptumo wanapitia. Namjua Sen. Cheptumo kwa sababu katika hapa Seneti amekuwa jirani kwa miaka hiyo miwili tukiwa hapa. Sio jirani yangu hapa tu, bali amekuwa jirani yangu pale katika gatuzi zetu. Laikipia na Baringo tunapakana. Kwa hivyo, yeye na mimi tumekuwa ni kama ndugu wa kufa kuzikana. Jambo ambalo tumekuwa tukiongea na yeye sana ni kuhusu usalama wa kaunti za Laikipia na Baringo haswa mambo ya hawa wezi wa mfugo. Aliniambia kwamba kile ambacho atafanya akiwa kama Mwenyekiti ni kujitolea kwa hali na mali ndio usalama uweze kupatikana katika Kaunti ya Laikipia. Nataka kumshukuru kwa sababu aliongoza Kamati yake mpaka Laikipia tukapata askari wa ziada. Kwa hivyo, nina kila sababu ya kumshukuru. Ninamkumbuka tukiketi pale, alikuwa ananiuliza mambo yalivyokuwa yakiendelea katika Laikipia. Leo nikiwa nimeketi pale, naona hayuko katika kile kiti. Mimi ninapatwa na huzuni kwa sababu kila wakati tulikuwa tukiongea na yeye sio tu, wakati kuna mijadala hapa kwa sababu yeye ni wakili aliyebobea, alikuwa ananipatia mawaidha kwa kuniambia vile ambavyo yeye anafikiria. Kwa hivyo, nina hofu na huzuni kwa kumpoteza rafiki na ndugu. Sikudhania itafika wakati huu niwe nikiongea hapa, kumwombeleza rafiki yangu na ndungu yangu, Cheptumo lakini lazima tukubali mambo ya Mwenyezi Mungu. Kile ambacho kinanifurahisha, hata ijapokuwa alikuwa na miaka 57 pekee, yale aliyoyatenda ni mengi. Amekuwa Naibu wa Waziri na Mwenyekiti wa kamati tofauti, hasa Kamati ya Usalama wa Taifa, Ulinzi na Mahusiano ya Kimataifa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}