GET /api/v0.1/hansard/entries/1518031/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1518031,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1518031/?format=api",
    "text_counter": 208,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, jambo hili limenifanya nikakumbuka ya kwamba sio miaka mingi ambayo utaishi dunia, ni vile ambavyo utakavyofanya ukiwa duniani. Nikisoma katika Kitabu Kitakatifu cha Mungu, Bibilia yangu inaniambia ‘naye Methusela akaishi zaidi ya miaka 900 lakini hakuna kitu alifanya isipokuwa kuishi duniani.’ Yesu aliishi miaka 32 duniani na alifanya mambo mengi. Kwa hivyo, ni vile ambavyo utakavyofanya ndio itakavyo kumbukwa. Sitaki kumsahau Mhe. Malulu Injendi, Mbunge wa Malava, kwa sababu alichangia Mswada wa Wazee wa Mitaani. Nakumbuka vizuri kwa sababu hawa wazee wanasaidia sana katika uongozi kule vijijini. Ni vizuri vile Injendi aliwaslisha Mswada huo. Itakuwa vyema tukiwapa kiinua mgongo wazee ambao wanafanyia wananchi kazi nzuri kule mashinani. Vile vile namkumbuka mimi na yeye tukiwa Wakatoliki. Tulifuatilia mambo ya dini pamoja. Kila wakati nilimwona amevaa rosari yake akitangaza wazi kuwa yeye ni Mkatoliki, haogopi na hana fedheha na akasimama hivyo. Mimi najua ya kwamba, hata wakati ameenda mbinguni wale walio mbinguni watamkiri kwa sababu na yeye alipokuwa duniani, alikiri imani ya Kanisa la Katoliki. Nashukuru, Bw. Spika wa Muda. Asante."
}