GET /api/v0.1/hansard/entries/1518049/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1518049,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1518049/?format=api",
"text_counter": 226,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kibwana",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 277,
"legal_name": "Kibwana Kivutha",
"slug": "kibwana-kivutha"
},
"content": "Asante, Bwana Spika wa Muda. Ninasimama hapa kuunga mkono wenzangu kwa kutoa rambirambi kwa kumpoteza shujaa mwenzetu, Seneta wa Baringo, Mhe. Cheptumo. Kwa niaba ya Kenya Women Senators Association (KEWOSA), ninatoa rambirambi. Sote kama akina mama wa KEWOSA tunasema pole kwa jamaa na marafiki wa Sen. Cheptumo. Kusema kweli, sikufanya kazi karibu na yeye lakini nilimjua. Tulifanya kazi kwa muda mfupi upande wa Kamati iliyochunguza mauaji ya Shakahola. Hapo niliweza kumjua vizuri na nikaelewa alivyoendesha kazi yake. Alikuwa mtu aliyependa uaminifu na kutaka kazi yake iwe safi ili kusibakie na kitu chochote au maswali ya kwa nini kazi haikukamilika vizuri. Sen. Cheptumo kusema kweli amekufa kishujaa. Ungemuuliza kwa nini anaonekana hajihisi vizuri, alikuwa akijibu kuwa yeye alikuwa sawa kabisa. Hakujihurumia na kwambia watu wengine kuwa hakujihisi vizuri. Kila mara alisema yuko sawa na wala hakuwa na ugonjwa wowote. Kwa kweli, amekufa kishujaa na ugonjwa wake bila kutaka watu wamwonee huruma. Kwa Kiislamu, sisi tunasema Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un” maana yake, The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}