GET /api/v0.1/hansard/entries/1518051/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1518051,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1518051/?format=api",
"text_counter": 228,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Okenyuri",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante sana, Bwana Spika wa Muda, kwa nafasi hii. Ninachukuwa nafasi hii kutoa pole zangu nikimwomboleza Sen. Cheptumo. Wakati mwingine nikiangalia maisha haya huwa ninashangaa kwa sababu mimi leo ninasherehekea siku ya kuzaliwa. Wakati huo pia ninaomboleza kumpoteza Sen. Cheptumo. Nikirejelea maneno ya William Shakespeare, alisema ulimwengu ni ukumbi wa michezo na kila mtu ana nafasi yake. Sen. Cheprtumo alikuwa na nafasi yake ya kuhudumia wakazi wa Baringo kwa miaka tulioitaja hapa. Kazi ya Mwenyezi Mungu haina makosa. Pengine ilikuwa mpango wa Mwenyezi Mungu kumpumzisha wakati huu. Kama viongozi wanaokuwa, tunajifunza kwa unyenyekevu ambao Sen. Cheptumo alikuwa nao. Tulikuwa tunakaa na yeye pale nyuma kama back benchers . Kipindi kingine aliniita na kuniuliza, “Okenyuri, umepangaje maisha yako? Nikiangalia naona kama ni baba ambaye alikuwa ananiona kama msichana mchanga na pengine alitaka kutoa wosia wake jinsi nitakavyojipanga katika mambo haya ya siasa na uongozi. Kwa hayo, nitamkosa sana. Ninaomba Mwenyezi Mungu alialaze roho yake mahali pema na kwa lugha ya Kikalejin- mutio mising."
}