GET /api/v0.1/hansard/entries/1518148/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1518148,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1518148/?format=api",
"text_counter": 31,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Ningependa kuwaambia kwamba, mtie masomo mbele na muendelee na hii kazi nzuri ambayo mnafanya. Hata ingawa mnasomea matibabu, nawajulisha kwamba mnaweza kuwa viongozi kama wale walio hapa. Kama vile Naibu Spika alifanya, alitaka muwe na maono na mawazo mazuri ya kuwatibu Wakenya wote. Nawatakia mema mkiwa hapa mkiona vile mjadala unaendelea katika Seneti hii. Mkirudi nyumbani, Meru, mseme hata sisi hapa tunamuenzi na kumpenda Naibu Spika wetu. Museme pia hata sisi tumempatia mamlaka hapa na mkirudi huko mmuombee na mmpe chochote anachotaka. Asanteni sana."
}