GET /api/v0.1/hansard/entries/1519595/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1519595,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1519595/?format=api",
    "text_counter": 350,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "na sifa ambazo tunamminia Mheshimiwa Raila Amolo Odinga kama mpeperushaji bendera katika Afrika kuwakilisha nchi ya Kenya. Mgala muue na haki umpe. Mheshimiwa Raila Amolo Odinga amekuwa kielelezo cha ustahimili wa demokrasia katika nchi ya Kenya. Amedhihirisha kujitolea mhanga kutetea haki za mnyonge wa nchi ya Kenya, kutuliza mawimbi ya kisiasa na vile vile kunyoosha mkono wa heri njema kwa wapinzani wake wa kisiasa tukitangulia na Marehemu Rais Daniel Arap Moi, Mwai Kibaki, Uhuru Kenyata na sasa Rais William Ruto. Hizi ni sifa za viongozi ambao kwao Afrika ilikuwa inaona nyota na nyota ilikuwa imeang’aa kule angani. Afrika imepoteza kiongozi shupavu aliye na msimamo na anayeheshimu itikadi na falsafa tofauti katika Afrika. Ni kiongozi ambaye anaelewa changamoto za watu wa Afrika; tajriba aliyonayo katika siasa za nchi ya Kenya na kwamba alikuwa mmojawapo wa viongozi katika Umoja wa Afrika aliyekuwa anashinikiza na kusimamia miundo mbinu katika Afrika na nchini humu. Mheshimiwa Raila Amolo Odinga amekuwa mtetezi wa haki za kibinadamu. Juzi, amepasua mbarika na kupeana msimamo wake kuhusiana na vifo na kupotea kwa Wakenya. Mheshimiwa Raila Amolo Odinga, na wengine vile vile amekuwa mmojawapo wa wale ambao wamekuwa wakishinikiza serikali za kipebari kubadilisha mfumo na kuongoza nchi zao kwa matawi na katika kufuata katiba za nchi hizo. Mheshimiwa Raila Amolo Odinga vile vile ameonyesha dunia nzima na Afrika kwamba ni lazima kufanya biashara kati ya nchi za Afrika, kuboresha uchumi wa nchi za Afrika. Hii ilidhihirika walipoungana na Mheshimiwa Mwai Kibaki kuleta mfumo mpya wa kiuchumi na kusisimua uchumi wa Afrika. Nimesikiliza Seneta wenzangu wakitaja na kupokezana makonde ya kisiasa kuhusiana ni nani ambaye anamfuata Raila Amolo Odinga kwa haki na matendo. Mimi ninaomba ya kwamba tusiwe vinanda vya kisiasa lakini tutende kulingana na maazimio ya Wakenya. Raila Odinga anashinikiza kuwe na demokrasia na vyama vya kisiasa. Viongozi walioko hapa lazima wasimame kidete na tuseme kwamba katiba inakubali vyama vya kisiasa. Katiba inakubali kwamba kuwe na uhuru wa kisiasa na mahusiano ya kisiasa. Ninataka kuona viongozi wenzangu chipukizi tunaposimama kando na kuwa vinanda vya kisiasa, sisi sasa tuwe watunzi wa nyimbo za demokrasia na kutetea hadhi na falsafa ya demokrasia katika nchi ya Kenya. Mheshimiwa Raila Amolo Odinga amepigana vita dhidi ya ufisadi. Ninaamini kuwa angetua uongozi wa jumuia ya Afrika angeongoza mapambano dhidi ya ufisadi katika nchi za Afrika. Changamoto nyingi zinazoendelea katika nchi za Afrika pamoja na vita vinavyoendelea ni kutokana na ufisadi. Mimi ninaomba kuwa, kutokana na Seneti tuone viongozi wakisimama kidete kupigana vita dhidi ya ufisadi katika nchi ya Kenya. Raila Amolo Odinga amedhihirisha kwamba kusulubiwa kisiasa sio mwisho wa safari. Aliwekwa korokoroni na akaondoka. Bibilia inasema Paulo na Sila waliomba milango ya gereza ikafunguliwa. Wengine wetu ni wajukuu wa kisiasa. Tumewahi kuwekwa korokorono na tukatoka. Kile tunataka kushukuru Mheshimiwa William"
}