GET /api/v0.1/hansard/entries/1519597/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1519597,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1519597/?format=api",
    "text_counter": 352,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Samoei Ruto ni kwamba alijitokeza mhanga akamshika mkono Mheshimiwa Raila Amolo Odinga. Viongozi wote wa upinzani na wasiokuwa wa upinzani walitembea na nyinyi katika baraste ya kuombea Mheshimiwa Raila Amolo Odinga afueni na atuee ushindi katika Afrika na nchi ya Kenya. Ninaomba tuendelee kufanya kazi na majadiliano kwa pamoja, na pia tupiganie haki za Mkenya na Afrika. Ipo siku itakakuja tutaulizwa yale tuliyoyatenda kwa mujibu wa Katiba na ujio wa siasa za nchi ya Kenya. Kwa hayo mengi, kwa niaba ya watu wa Jimbo la Bungoma, watu wa Mkoa wa Magharibi na Chama cha Kisiasa na ambacho kimebobea na kina ukomavu mkubwa wa kisiasa, chama cha FORD-Kenya; chama kilichokuwa uwasisi wa demokrasia katika nchi ya Kenya, tunampa heko na kongole Mheshimiwa Raila Amolo Odinga kwa kupeperusha bendera ya nchi ya Kenya. Pia, tunamshukuru Rais William Ruto kwa kujitokeza mhanga kama Rais wa nchi ya Kenya na kutembea na Mkenya mwenzake. Ningewaomba wale wenzangu ambao wana wivu na inda mioyoni mwao kuhusiana na Raila Amolo Odinga, iwapo hauwezi kupiga hatua mbele, usimwonee mwenzio aliye na hesabu na uwezo wa kupiga hatua mbele kwa sababu hatua hiyo ndiyo Kenya inastahili kuchukua ili tulete ukombozi na urejesho katika nchi yetu. Mheshimiwa Raila Amolo Odinga ninakutakia maisha mema unapoendelea kuongoza mchakato wa demokrasia na kuungana na Mheshimiwa William Ruto. Sitaki kumsahau papa wa Roma, Spika wa Bunge la Kitaifa, ambaye yuko papo hapo kuhakikisha Kenya inasonga mbele. Asante sana na Mungu awabariki."
}