GET /api/v0.1/hansard/entries/1519729/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1519729,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1519729/?format=api",
    "text_counter": 118,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
    "speaker": null,
    "content": " Asante Mhe. Spika. Kwa hakika ni pigo kubwa sana kwa Taifa letu la Kenya na pia kwa Mabunge yetu mawili kupoteza viongozi wetu wawili mashujaa. Mhe. Cheptumo alikuwa Seneta wa Baringo. Alikuwa kiongozi mwenye busara sana. Alikuwa kiongozi mwadilifu na hata wakati alipokuwa akichangia Miswada na Hoja katika Bunge hili la kitaifa, ungemwangalia na ungejua alikuwa kiongozi ambaye anajielewa na anajua kwa nini ako katika Bunge hili la kitaifa. Mheshimiwa huyu alitoa mchango mkubwa sana hata kule nyanjani. Tumezungumza na watu wengi sana kutoka sehemu ya Baringo na wanasema ameliacha pengo kubwa. Kwa niaba ya watu wa Likoni, poleni sana. Mwenyezi Mungu apatie familia na Taifa la Kenya faraja. Ndugu yetu Mhe. Malulu Injendi pia alikuwa kiongozi muadilifu na shupavu. Kakamega ni sehemu ambayo Chama cha Chungwa kimebobea lakini alichaguliwa akiwa katika Chama cha UDA. Kwa hivyo, ni kumaanisha ni kiongozi ambaye alikuwa anatenda mema na anafanya mambo zaidi haswa katika mambo ya miradi. Ni Mheshimiwa ambaye alikuwa mpole. Hata kwa kumuona, alikuwa anavaa msalaba shingoni ishara kuwa yeye ni mkatoliki. Kwa hivyo, Taifa la Kenya na Mabunge yetu yamepoteza viongozi shupavu. Haswa Hon. Malulu alichangia pakubwa katika elimu. Na Mhe. Cheptumo alichangia sana katika zile kamati alizokuwa mwanachama, haswa ile Kamati ya Maswala ya Kisheria."
}