GET /api/v0.1/hansard/entries/1520124/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1520124,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1520124/?format=api",
"text_counter": 115,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Mhe. Ruweida Mohammed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": " Ahsante, Mhe. Naibu wa Spika, kwa kunipatia nafasi hii ya kuchangia Mswada huu. Mswada huu wa mfuko wa kusawazisha utahakikisha kuwa yale maeneo bunge yaliyokuwa chini yatainuliwa yawe sawa na mengine. Sheria hii inavyopangiwa itasaidia sana. Hapo awali, mfuko huo ulikuwa na pesa lakini hapakuwa na sheria, kwa hivyo pesa zilifujwa. Sheria hii itatusaidia ili mambo yafunguke na maeneo yetu yawe kama maeneo bunge mengine. Usimamizi wa pesa hizo ni muhimu. Ninaweza toa mifano. Mara ya kwanza pesa zilipotoka, Eneo bunge langu lilipata Ksh120,000,000 zilizotumika kutengeneza barabara ya kokoto inayoitwa Mtangawanda-Kizingitini. Kulikuwa na kampuni inayoitwa Zarara Oil and Gas Company iliyokuja kutafuta gesi ambayo pia ilitengeneza hiyo barabara. Ni kama nusu ya barabara hiyo ilitengenezwa na Zarara Oil and Gas Company na nusu ikatengenezwa na"
}