GET /api/v0.1/hansard/entries/1520126/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1520126,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1520126/?format=api",
"text_counter": 117,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Mhe. Ruweida Mohammed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": ". Lakini ukweli wa mambo ni kuwa pesa hizo zilifujwa. Cha kusikitisha ni kuwa kwa sababu barabara ni ya kokoto, haikufuatiliwa kwa sababu wangesema kuwa mvua ilinyesha na kwa hivyo pesa zilitumika. Ningependa kutoa pendekezo kuwa pesa hizo zisitumike kujenga barabara za udongo. Zitumike kujenga barabara ya lami, hata kama ni kilomita moja, kuliko kutumika kwa njia ambazo mtu anaweza jificha nazo azimalize. Pesa hizi ni za maskini. Watu wanasahau kuwa pesa za maskini zikiliwa, humrudia mtu. Kama pesa hizi zingetumika kwetu, tungekuwa mbele sana na tungekuwa tunatumia hizi pesa zingine kusonga mbele zaidi. Kwa mfano, watu wa Mangai walio katika Msitu wa Boni waliwekewa Ksh45,000,000 za maji. Mradi huo ungekuwa umeinua eneo hilo. Tangu tupate Uhuru, eneo hilo halijakuwa na mradi hata mmoja wa Serikali. Mradi mkubwa saa hii ni huu niliouanzisha wa kujenga shule nikisaidiwa na Kenya Defence Forces (KDF). Lakini ukitafuta pesa hizo Ksh45,000,000 zilizofujwa, hutajua ziko wapi wala zilifanya nini. Hazikutumika. Mpaka sasa, pesa hizo hazijulikani ziko wapi. Lakini sheria hii ikiwekwa, itatusaidia."
}