GET /api/v0.1/hansard/entries/1520127/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1520127,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1520127/?format=api",
    "text_counter": 118,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Mhe. Ruweida Mohammed",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Tukizungumzia kuhusu pesa hizi, kila mtu anafikiria ubinafsi. Ukweli ni kuwa wale wanaoishi kule kwingine ni ndugu zenyu. Kama vile pesa zinawekwa katika miradi ya chai au kahawa, msikasirike zikiwekwa huko kwingine. Sisi hatukasiriki kwa sababu hatuna chai kwa hivyo hatuwezi lilia pesa hizo. Pesa za marginalisation ni za kurekebisha makosa yaliyotokea katika serikali zote zilizopita. Hiyo sio pendeleo tunafanyiwa. Ninamshukuru Rais kwa sababu tangu aingie mamlakani miaka miwili iliyopita, amefanya zaidi ya pesa zilizowekwa. Ukihesabu faida ya pesa hizi, hazilingani na alichofanya. Kwa mfano, Rais anaweka lami kilomita 15 katika barabara ambayo pesa za Equalisation Fund zilifanyiwa ubadhirifu. Mbona hakusema atajenga kilomita thelathini na tano? Amesema atafanya kitu kitakachoonekana. Watu walio na miaka arubaini ama sitini waliozaliwa Lamu Mashariki ambao kutoka wazaliwe, hawajawahi kuona barabara, hata nao waione. Ninataka Wabunge wenzangu waelewe kuwa maeneo yetu ni tofauti na maeneo yao. Katika Pwani, maeneo bunge mengine ni tofauti na yetu. Kwa mfano, mtoto akizaliwa Voi anaona reli na barabara. Si lazima aende safari ili aone barabara. Mtoto anayetoka Lamu Mashariki lazima aende safari akiwa shulen ili aone barabara ya lami. Rais huyu ndiye ametambua kuwa kuna"
}