GET /api/v0.1/hansard/entries/1520130/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1520130,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1520130/?format=api",
    "text_counter": 121,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Mhe. Ruweida Mohammed",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Watu katika maeneo bunge yetu wanataka tumaini. Roho zao zilikuwa zimekata tamaa na hawakuwa na tumaini katika Kenya. Rais wetu ametupa tumaini. Watoto wetu wana tumaini kuwa barabara zitajengwa. Leo tumetia sahihi katika mkataba wa kihistoria. Kutoka mwanzo wa dunia, kati ya vijiji vyangu ishirini na tatu, vijiji kumi na mbili pekee vina stima. Saa hii, tumetia sahihi mkataba katika vijiji vitatu, yaani, Ndau, Kiwayu na Mkokoni ili ziwekwe mini grid za solar . Jambo hilo limenifanya niwe very emotional. Karibu nilie katika mkutano huo. Watu wangu na watoto wao hawajawahi ona stima kwa miaka hii yote ilhali tumekuwa tukifanya CBC. Hii CBC inafanyika vipi kule kama hata shule hazina stima? Tukizungumzia haya, watu wengine wanaona ni kama tunapenda kulalamika. Kamati la Bunge hili lilienda kule na wakaniambia kuwa walikuwa wanaona ikiwa maeneo bunge yao yako nyuma lakini kuna maeneo bunge mengine yana shida. Ukienda kwangu, Mhe. Naibu wa Spika, utatumia ndege, mashua, gari na pikipiki. Wakati mwingine kama uko na walinzi, watakuonya kuwa kuna sehemu ambazo huwezi kuenda. Nilienda na kamati mbili na wakakatazwa kufika Mangai. Barabara ni mbovu na kuna ukosefu wa usalama. Kwa hivyo, ninawaomba ndugu zangu kuwa tupitishe Mswada huu na marekebisho ili uweze kusaidia maeneo yetu. Ukisaidia maeneo yetu, pia utasaidia maeneo yenyu. Ukienda kule Kiangwi, kuna kituo cha polisi na hospitali. Ndugu zenyu wanafanya kazi kule. Haimaanishi kuwa ni Mbajuni pekee yake ndiye atakayepata shida. Polisi wakipelekwa sehemu kama Kiwayu wanakuwa wazimu baada ya miaka mitano kwa sababu ya hali ngumu ya maisha. Hao ni watoto wenyu. Sio watoto wa Kibajuni pekee walio huko. Kuna watu wa makabila tofauti tofauti wanaoenda huko kama madaktari au polisi. Ni lazima maeneo yale yainuke ili watu wakija kufanya kazi kule, wasiwe na shida nyingi, na waweze kufanya kazi vizuri."
}